Tuesday, 20 June 2017

MKUDE AFUNGUKA YA MOYONI

KIUNGO Jonas Gerald Mkude amesema anafurahia maisha Mtaa wa Msimbazi ndiyo maana ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC.
Akizungumza na CHENGULA NEWS, Mkude amesema kwamba anashukuru baada ya vikao mfululizo na uongozi wa Simba wamefanikiwa kufikia maafikiano, ambayo ni kuongeza mkataba wa miaka miwili.
“Ninashukuru baada ya vikao vikao na viongozi tumefanikiwa kufikia makubaliano mazuri. Nataka niwape habari nzuri wana Simba, nitaendelea kuwa nao kwa miaka mingine miwili,”amesema Mkude.

Nahodha huyo wa Wekundu wa Msimbazi, amesema kwamba kuongeza mkataba Simba ni changamoto nyingine kwake, kwani anatakiwa kuendelea kudhihirisha ubora wake Msimbazi na kuisaidia timu.
Amesifu jitihada za uongozi kuboresha kikosi kwa kusajili wachezaji wazoefu na kuwapa mikataba mipya wachezaji waliopo ambao ama wanamaliza au wanakaribia kumaliza.
“Unapotaka kujenga timu kwanza lazima uwalinde wachezaji wako wazuri ulionao, na pili usajili wapya wanaohitajika kuja kuimarisha kikosi, ndiyo maana ninawapongeza viongozi,”amesema. 
Mkude aliibukia kikosi cha pili cha Simba mwaka 2011 kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2012 na tangu mwaka 2013 amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza cha Wekundu hao wa Msimbazi. 

NIYONZIMA AWADUWAZA YANGA SC CLOUB

Na PAUL CHENGULA

    Kiungo matata maarufu kama niyonzima,amezidi kuwashangaza wapenzi na mashabiki wa club ya dar yanga africa jijini dar esalam.

Nibaada ya mkanganyiko mkubwa uliokuwepo juu ya hatma yake ya kurudi dimbani katika msimu ujao wa 2017-2018
 
Kiungo huyo machachari ameweka wazi kuwa yupo tayari kuitumikia club ya simba na ameweka wazi juu ya mawasiliano na simba juu ya kujiunga na kikosi cha simba katika msimu ujao

Thursday, 27 October 2016

KAULI MPYA YA SERIKALI SIMBA,YANGA,KUKODIHWA.

Image result for simba scSERIKALI imewashauri wafanyabiashara vijana, Mohamed 'Mo' Dewji na Yussuf Manji kuanzisha timu za kama mfanyabishara mwenzao mwenye asili ya Kiasia agiza, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa kuliko kuzing'ang'ania Simba na Yanga.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja alipozungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dart es Salaam kuhusu fukuto la mabadiliko Simba na Yanga.
Kiganja kwanza ameagiza kusitishwa michakato yote inayoendelea ya kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa Wanachama kwenda katika umiliki wa hisa na ukodishwaji kwa Klabu za Simba na Yanga hadi kutakapofanyika marekebisho ya katiba zao.Image result for yanga sc
Amesema klabu hizo zinapaswa kurekebisha katiba zao kwanza kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9) .
Kiganja alisema kuwa mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye Klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kupinga michakato hiyo kitu ambacho sio kizuri na pia sio ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.Image result for simba sc
"Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa Wanachama kwenda kwa uwekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapo fanya mabadiliko kwa mujibu wa Katiba za Klabu zao," alisema Kiganja.
Aidha BMT imemtaka mdau au mwanachama yoyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye Klabu hizo ni vema angeanzisha timu yake kama Saidi Salum Bakhresa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko kwavile timu hizo zina Wanachama wengi.
Kiganja alisema kuwa michImage result for yanga scakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote kwani mabadiliko yoyote ndani ya klabu hizo lazima yafuate Katiba zao.
Manji anataka kuikodisha Yanga kwa miaka 10, wakati Dewji anataka kununua asilimia 51 ya hisa

Thursday, 8 September 2016

MIUJIZA MIPYA YAJITOKEZA JIJINI DAR ES SALAAM

Nimiezi mitatu toka usafiri huu maarufu mjini kama bodaboda kuwepo katika viwanja hivi vya vetenari

Kwa mujibu wa shuhuda wetu ameieleza chengula news,  muhusika wa pikipiki hii amefariki dunia baada ya kuanza kuitumia kama usafiri wa kibiashara mahali hapa

Taarifa za mashuhuda zinasemakuwa bodaboda hii iliibiwa kutoka tanga na kuletwa daresalaam kwaajili ya biashara hatahivo pikipiki hiyo imekuwa na maajabu mengi jambo ambalo wausika wamekuwa wakilinganisha na ushirikini

CHENGULA NEWS ilivyo zungumza na wausika wamesema kuwa pikipiki hiyo haisogei wala haitoki jambo ambalo limekuwa kama utalii kwa wakazi wa jiji la daresalam kufika eneo husika na kujaribu kuitoa pikipiki

Monday, 5 September 2016

SIMBA SC FITI KUIVAA RUVU SHOOTI



Kikosi cha Simba kilichokwenda mkoani Dodoma kujiweka sawa kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara, kimerejea jijini Dar es Salaam jana Jumapili na kutamba kuwa ipo ‘full tank’ kwa ajili ya kutoa dozi katika mechi zilizo mbele yao.

Simba ilikwenda mkoani humo baada ya kupata mwaliko wa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hata hivyo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda, Jackson Mayanja, amesema kwamba kupata safari hiyo pamoja na kucheza mchezo huo wakati ligi kuu imesimama, imekuwa ni faida kubwa kwao katika kujiweka sawa na kurekebisha waliyoyaona katika mechi zao mbili za awali, hivyo sasa wamekuwa fiti zaidi katika kila sekta.

“Mazoezi na mechi tuliyocheza Dodoma imekuwa na mchango mkubwa kwa maandalizi na kujiweka fiti zaidi kwa ajili ya michezo inayokuja, imekuwa vyema kupata nafasi ya kuja sehemu kama hii wakati ligi imesimama na kupata muda wa kurekebisha tuliyoyaona kwenye mechi za awali za ligi.

“Bado safari ni ndefu na ligi ina mechi nyingi, kwa hiyo unapopata nafasi kama hii na unapoitumia vizuri, inaleta faida kubwa kwa mechi za baadaye, ukizingatia msimu huu tunahitaji kufanya vizuri zaidi,” alisema Mayanja.


Mpaka sasa, Simba imecheza mechi mbili za ligi, ya kwanza waliumana na Ndanda na kushinda kwa mabao 3-0, mechi ya pili wakatoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu, jumla imekusanya pointi nne. Keshokutwa Jumatano wanatarajia kucheza dhidi ya Ruvu Shooting

Thursday, 21 July 2016

SAMATA AITIKISA ULAYA KRC GNK YAIBUKA

Mtanzania Mbwana Samatta bado anaendelea kufanya vizuri na kuzidi kuaminiwa na kocha wake Peter Maes ambaye kwa sasa amekuwa akimpa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na kucheza dakika zote 90, usiku wa July 21 2016 Mbwana Samatta aliichezea KRC Genk mchezo wa pili wa Europa League dhidi ya Buducnost ya Montenegro.
Genk imecheza mchezo wake wa pili na kulazimishwa kucheza kwa dakika 120 na baadae mikwaju ya penati, dakika 120 zilimalizika kwa Buducnost kuongoza kwa goli 2-0, goli ambazo zilifungwa na Djalovic dakika ya 2 na Raickovic dakika ya 40 lakini mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati kutokana na KRC Genk kuibuka na ushindi kama huo katika mchezo wao wa kwanza.
Katika mikwaju ya penati Genk imefanikiwa kuibuka  na ushindi wa penati 4-2, penati za ushindi wa Genk zilipigwa na nahodha wao Thomas Buffel, Heynen, Mbwana Samatta na Walsh, hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk itacheza round ya pili ya Europa League dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland.

Friday, 15 July 2016

SHAA AFUNGUKA KUJITOA MJ RECORDS

Ni July 15, 2016 ambapo Malkia wa uswazi, Sara Kaisi aka Shaa amefunguka kupitia  chengula news na kuelezea sababu za kuondoka kwenye uongozi wake wa zamani.
Akizungumza na chengula news staa huyo alisema…’Nimekuwa na ndoto ya muda mrefu kama ya miaka mitano iliyopita tumeona wasanii ambao niliokuwa nao MJ Records wakina Izzo Bizness amesimama mwenyewe ukija kwa Quick Rocka nae kafungua studio kwahiyo huu ni muda wangu’Shaa
‘Maamuzi ya mimi kwenda kwenye uongozi wakina Tale ilikuwa baada ya mimi mkataba wangu kumalizika kwenye lebo ya Unity Entertainment ya AY nilifanya nao kazi nzuri mpaka zingine zikakubalika ila maamuzi yangu kwa 2016 kazi zangu zitasimamiwa chini ya record label yangu’- Shaa