Katika gazeti la changamoto katika ukurasa wake
wa kwanza unasomeka "Zitto azidi kuwaumiza CHADEMA" na habari hiyo ukiifuatilia
ndani inaeleza kuhusu kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe na jinsi Zitto
alivyoipokea.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba, Zitto hakutarajia mtu
ambae yeye anamuheshimu katika siasa kuwa na misimamo isiyo tanguliza maslahi ya
taifa mbele na badala yake kushikilia matatizo yao yaliyojitokeza huko nyuma
ambayo kimsingi yalihusu nafasi za kiuongozi.
Zitto alieleza kuwa kwa
sasa hayupo tayari kujibizana na viongozi tena kwa kuwa amekuwa akisema hivyo
kila mahali anapokwenda kufanya mikutano yake na amewekeza nguvu nyingi katika
kukitangaza chama chake kipya. Pamoja na malengo hayo, ila kwa kauli ile ya jana
ameona hana budi kuitolea maelezo!
Zitto alisisitiza kuwa matatizo yake
binafsi na viongozi wa chama chake cha zamani yasipewe kipaumbele kuliko maslahi
ya taifa. Ameeleza kuwa mara kadhaa ameomba chama chake kijiunge na UKAWA lakini
CHADEMA wamekuwa wakigoma. Kauli ile ya jana sio ngeni masikioni pangu. Alieleza
Zitto.
Zitto aliongezea kuwa, "kama ni matatizo basi ni kati yangu na
viongozi wa CHADEMA na yasifanywe ya taifa zima. ACT-Wazalendo tuna nia ya dhati
ya kuwaondoa CCM madarakani. Pia UKAWA wana nia hiyo hiyo. Kwa hali hiyo hatuna
budi kushirikiana kummaliza CCM na hilo litafanyika kama kweli tumetanguliza
utaifa mbele badala ya matatizo yetu binafsi na viongozi wa chama changu cha
zamani."
My Take,
Zitto amekomaa kisiasa na ana ngozi ngumu sana.
Pamoja na mihasira na Mbowe na maneno yake ya ovyo kuhusu Zitto, lakini kijana
Zitto amemjibu kistaarabu sana na bado ameonyesha nia ya kutaka ushirikiano na
UKAWA.
No comments:
Post a Comment