CAMP Nou ni sehemu ya machinjio! hivyo
ndivyo unavyoweza kusema baada ya Barcelona kuichapa Getafe magoli 6-0 katika
mechi ya ligi kuu Hispania, La Liga iliyomalizika usiku huu.
Mapema dakika ya 9′ Lionel Messi
aliandika goli la kuongoza kwa mkwaju wa penalti na katika dakika ya 25′ Luis
Suarez alipiga bao la pili.
Dakika ya 28′ Neymar Jr akapiga goli la
tatu na chuma cha nne kimetiwa kambani na Xaiv Hernandez.
Suarez alitikisa tena nyavu dakika ya
40′ akifunga goli la tano na Messi akamaliza shughuli dakika ya 47′ akifunga
goli la sita
No comments:
Post a Comment