Tuesday 28 April 2015

LIGI YA MIKOA YANUKIA

Na Paul chengula














LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) sasa itaanza Jumamosi Mei 9, 2015 badala ya Jumamosi Mei 2, 2015 kama ilivyokua imetangazwa awali.
Uamuzi huo umefanyika ili kutoa fursa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukamilisha maandalizi ya mwisho ikiwemo ukaguzi wa viwanja ambavyo vitatumika katika RCL na masuala mengine ya kumsingi.
Tunaomba radhi kwa usumbufu ambao utakuwa umejitokeza kutokana na taarifa hii ya kusogeza mbele kuanza kwa ligi, lakni pia kuzitakia kila la kheri timu zinazoshiriki katika maandalizi yao. Ratiba ya mashindano itatolewa/kutumwa leo kama ilivyopangwa awali

No comments:

Post a Comment