Gabon ndiye mwenyeji wa kombe la mataifa ya Afrika yatakayoandaliwa mwaka wa 2017.
Gabon imeahidi kutumia viwanja 4 katika mashindano hayo yenye timu 16 kati ya mwezi Januari na Februari.Viwanja hivyo vitakuwa Libreville Franceville, vilivyotumika mwaka wa 2012,huku Port Gentil na Oyem
zikitarajiwa kukamilishwa katika kipindi cha miezi 14 ijayo kwa mujibu wa onyesho la shirikisho la soka la Gabon.
Gabon, inayopewa nafasi ya kushinda kinyang'anyiro hicho, iliandaa kwa pamoja na majirani zao Equatorial Guinea, fainali za mwaka 2012
Wenyeji wa awali wa fainali hizo, Libya, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekwamisha shughuli za mpira, ilijitoa mwaka jana kuandaa mashindano hayo.
Kamati ya shirikisho la vyama vya soka barani Afrika, Caf, itaendesha uteuzi huo katika mkutano wake wa mwaka utakaofanyika mjini Cairo,
Misri kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo.
No comments:
Post a Comment