STAND United ya Shinyanga inainyatia saini ya kipa wa
zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja, imeelezwa.
Mkurugenzi wa benchi La Ufundi wa Stand United, Muhibu
Kanu ameiambi ,chengula newz, jana kwamba, wana mipango ya kumsajili kipa huyo wa
zamani wa Simba na Yanga, Juma Kaseja kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara.
“Kaseja ni kipa mzuri, mzoefu ambaye tunaamini bado
ana uwezo mkubwa na atatusaidia tukiwa naye,”alisema.
Kwa sasa, Juma K Juma ni mchezaji huru baada ya
kujiondoa katika klabu yake, Yanga SC akiishutumu kukiuka vipengele vya Mkataba
baina yao. Hata hivyo, Yanga SC imemfungulia kesi Kaseja ambayo inaendelea
Mahakama ya Kazi.
Kwa upande wake, kocha wa Stand United, Mganda Mathias
Lure amesema kwamba ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili umeamsha
morali ya wachezaji wake na sasa watapambana zaidi wasishuke.
"Mechi yetu ijayo itakuwa siku ya Jumapili na
tunacheza na Polisi Morogoro, kisha tunabakiza mechi sita, dhidi ya Ruvu
Shooting, JKT Ruvu
tukiwa nyumbani na ugenini tutacheza na Azam, Yanga na
Coastal Union,”amesema Luren ambaye timu yake ipo katika nafasi ya 11 kwenye
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24.
No comments:
Post a Comment