Linahesabika
kama tukio jingine la Basi kuwaka moto katika rekodi za mabasi
yaliyowaka moto yakiwa safarini nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu baada ya kuongea na CHENGULA NEWZ
ni kwamba basi hili la kampuni ya Dar Express liliwaka moto likiwa
safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa abiria.
Amesema >>> ‘Ni
kweli basi la Dar Express saa saba mchana kwenye kijiji ndani ya Wilaya
ya Bagamoyo Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati
nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote,
hawakuwahi kulizima, hakuna yeyote aliejeruhiwa‘
No comments:
Post a Comment