Saturday 9 May 2015

MABONDIA 10 MATAJIRI ZAIDI DUNIANI

may

CHENGULA NEWZ

 Mchezo wa ngumi ni mmoja ya michezo maarufu na inayopendwa zaidi duniani.
Pambano la May 2 2015 kati ya Floyd Mayweather na mpinzani wake Manny Pacquiao lilidhihirisha kwamba kumbe kuna mashabiki wengi duniani wanaopenda mchezo wa ngumi.
Forbes imetoa orodha ya mabondia ambao wanaongoza kwa utajiri mkubwa zaidi duniani;
No.1- Floyd ‘Money’ Mayweather: Mbabe huyu ndio tajiri  zaidi kwa mabondia duniani.. Utajiri wake ni kama dola Mil. 380. 
pil
No.2: George Foreman: Anashika nafasi ya pili kwa utajiri kwa utajiri wa dola Mil. 250, alistaafu ngumi za kulipwa kwa sasa ni mjasiriamali na mwigizaji.
osc
No.3- Oscar De La Hoya: Utajiri wake ni dola Mil. 175, mpaka anastaafu mwaka 2009 alikuwa na ushindi wa mapambano 39 kati ya 45 aliyowahi kucheza. Huyu ni raia wa Mexico.
mx
No.4- Lenox Lewis: Jamaa ana uraia wa Uingereza na Canada.. Utajiri wake ni kama dola Mil. 140 hivi, aliingia kwenye headlines baada ya kuwapiga mabondia kama Mike Tyson mwaka 2002.
ppp
No.5: Emmanuel ‘Manny’ Dapidran Pacquiao: Raia wa Ufilipino ambae aliingia kwenye headlines baada ya kupigwa na bondia Mayweather May 2 2015 Marekani.. Bado yuko vizuri kwenye nafasi ya tano na utajiri wake wa dola Mil.120.. mapato yake yanatokana na mchezo wa Ngumi, matangazo ya biashara, pamoja na posho za Ubunge nyumbani kwao Ufilipino.
ray
No.6- Sugar Ray Leonard: Ni bondia Mmarekani aliyestaafu akiwa na record kubwa pia, katika mapambano yake 40 alishinda jumla ya mapambano 36. Baada ya kustaafu mwaka 1997 aliamua kujishughulisha na uchambuzi wa Michezo pamoja na kucheza movies.
kli
No.7- Vitali Klitschko: Utajiri wake ni kama dola milioni 65. Jamaa baada ya kustaafu boxing akaamua kuingia kwenye siasa, kwa sasa ni Meya wa Jiji la Kiev, nyumbani kwao Ukraine.
muu
No.8- Muhammad Ali: YES.. Dunia inatambua record ya huyu bondia, kwa sasa anashighilisha na masuala ya Harakati za Mambo ya Kijamii Marekani.. Utajiri wake ni dola Mil. 50. Moja ya aka alizowahi kupewa ni The Greatest.
tsa
No.9- Marvin Hagler: Ni bondia wa Marekani ambaye alistaafu akiwa na record ya kushinda mapambano 62 kati ya 67 aliyowahi kucheza. Baadae akaingia kwenye ishu ya kucheza movie.. Utajiri wake ni dola Mil. 45
hop
No.10- Bernard Hopkins: Jamaa aka yake anaitwa The Executioner, ni bondia ambaye anapigana ngumi za ubingwa wa dunia kwa uzito wa kati, ana utajiri wa dola Mil. 40

No comments:

Post a Comment