Na Paul Chengula
MWANAMKE ajulikanae kwa jina la mwasiti juma ,mkazi wa songea ameelezea matatizo yalio mkuta siku alipo unguzwa na mumewe ajulikanae kwa jina la muhammed ally mkazi wa songea vijijini,kisa pombe
mwanamke huyo ambae amekutwa na mkasa huo ambapo alipokutwa na mumewe nyakati za usiku wakati yeye akihudumia nguruwe kwa kutoa uchafu kwenye boma la nguruwe
ndipo alipoingia mume wake na kumtaka aache kazi alizokuwa akizifanya na kumfata jikoni ambapo mwasiti alikuwa amembandikia mumewe maji ya kuoga ,mume huyo ndipo alipo anza kumshutumu mama huyo kwa kosa la kuchelewa kupika mpaka muda anao fika yeye kwanini hajamaliza kupika
Pia baada ya kumsema mwasiti ndipo baba huyo alipo amua kuchukuwa sefuria la maji lililo kuwa jikoni na kumwagia mama huyo ambae alikuwa amejifunga kitenge
Mashuhuda wa tukio hilo walipo zungumza na CHENGULA NEWZ walisema kuwa baba huyo amekuwa akimtukana mwasiti kila anapo kuwa akirudi nyumbani ambapo maranyingi huwa anarudi akiwa amelewa ,pia majirani waliiambaia CHENGULA NEWZ kuwa baba huyo ni balozi wa nyumba kumi katika kijiji chao hivyo mwasiti amekuwa akipigwa na kukosa sehemu ya kupeleka matatizo yake.
No comments:
Post a Comment