MFUNGAJI
bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva anarejea jioni
ya leo Dar es Salaam na tabasamu ‘kuubwa’ baada ya kufaulu majaribio ya
kucheza soka ya kulipwa Afrika Kusini.
Winga
huyo wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC jana amekamilisha majaribio
yake ya siku tatu Bidvest Wits ya Ligi Kuu nchini humo na matokeo ni
‘safi’.
CHENGULA NEWZ inafahamu Bidvest Wits wameridhika na uwezo Msuva na sasa wanafungua majadiliano na klabu yake, Yanga SC.
Msuva
amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake Yanga SC na Wits iko tayari
kutumia si zaidi ya dola za Kimarekani 100,000 (Sh. Milioni 200)
kukamilisha dili zima la mchezaji huyo- kwa maana ya malipo ya mchezaji
kusaini na ada ya uhamisho kwa klabu yake.
Msuva
aliondoka Dar es Salaam Jumatano wiki hii akiwa tayari ameipa Yanga SC
ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, huku pia akiwa anaongoza kwa mabao, 17
akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Amissi Tambwe mabao 14.
Amekosa mechi mbili za mwisho dhidi ya Azam FC Yanga ikilala 2-1 na leo
dhidi ya Ndanda ya Mtwara.
Tangu
ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 akitokea Moro United, Msuva ameifungia
timu hiyo mabao 35 jumla katika mechi 102 za mashindano yote
No comments:
Post a Comment