Hivi karibuni Burundi imeingia kwenye
headlines kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo
kufuatia Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania nafasi ya Urais kwa awamu ya tatu .
Leo Stori mpya kutoka Burundi ni Jeshi
la nchi hiyo kuamua kumpindua Rais huyo madarakani ili kuondokana na
machafuko ambayo tayari yameua baadhi ya watu huku wengine wakikimbilia
katika nchi za jirani.
Meja Generali mstaafu wa jeshi la Burundi Godefroid Niyombareh na kamati yake walifikia maamuzi hayo kwa madai amekosa vigezo baada ya kuonekana kukataliwa na kukiuka katiba ya nchi hiyo
Mapinduzi ya kumtoa Rais huyo yamefanyika leo wakati akiwa Tanzania akijumuika na viongozi wengine wa Afrika Mashariki akiwemo Museni na Kagame kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea nchini humo.
Wananchi mbalimbali nchini humo
walionekana kupokea taarifa hiyo kwa furaha kubwa na kupita sehemu
mbalimbali huku wakishangilia.
No comments:
Post a Comment