Wednesday, 20 May 2015

YANGA YAIMALIZA SIMBA TENA

Salim Mbonde
Na Paul chengula, Dar es Salaam
 
 
‘Mbonde amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu kiasi cha kuwatoa udenda Simba na Yanga.’
MECKY Mexime, kocha mkuu wa Mtibwa Sugar FC, amesema hawezi kumzuia beki wake tegemeo Salim Mbonde kujiunga na klabu kongwe za soka nchini, Simba na Yanga zinazomtaka.
Akiwa Morogoro leo mchana, Mexime amesema anatambua kuwa nyota wake wanahitaji kuwa na maisha mazuri, hivyo hawezi kuwa kikwazo kwa kuwazuia kujiunga na timu zinazotaka kuwapa maisha mazuri zaidi ya yale wanayoyapata Mtibwa.
“Soka ni maisha. Mchezaji anapopata timu inampa maslahi mazuri, siwezi kumzuia. Bado hatujapokea ofa kutoka kwa timu yoyote kuwataka wachezaji wetu ambao bado wana mkataba na Mtibwa,” amesema Mexime.
Mkataba wa Mbonde na Mtibwa Sugar umemalizika huku nyota huyo akitaka alipwe Sh. milioni 30. Tayari Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope, imeshatangaza kuachana na mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko Afrika Kusini akikitumikia kikosi cha Taifa Stars katika michuano inayoendelea ya Cosafa.

No comments:

Post a Comment