Ligi Kuu TZ bara inatarajiwa kuanza
August 2015, Vikosi ya Timu za soka vimeendelea kujipanga na kuimarisha
Vikosi vyao ili mambo yaende sawa msimu huu watoke na ushindi, Azam FC wamethibitisha kwamba safari hawako tayari kuukosa pia.
Azam FC jana
ilithibitisha kuanza kuwapokea wachezaji wa kigeni
wanaotarajia kujiunga nao na kufanya majaribio na klabu hiyo, kwenye
taarifa ya Klabu hiyo imeonesha jana usiku walitarajia kumpokea golikipa
ambaye ni raia wa Cameroon, Nelson Lukong Bongaman ambaye alikuwa anachezea timu za Congo DRC.

Jean Mugiraneza Babtiste
Klabu hiyo ilitarajia pia kumpokea staa mwingine mida ya saa 2 asubuhi ambae ni raia wa Uingereza, Ryan Burge.
Nyota mwingine waliyemtaja kuwa watampokea ni mchezaji kutoka Klabu ya APR ya Rwanda, Jean Mugiraneza Babtiste.
Kikosi cha Azam FC kimeelekea Tanga kwa ajili ya maandalizi ya kukipiga na Klabu ya African Sport kwenye mchezo wao wa kirafiki siku ya Jumamosi katika Uwanja wa CCM Mkwakwani na Jumapili watakuwa na mchezo na Klabu ya Coast Union.
No comments:
Post a Comment