
Siku kadhaa baada ya kumaliza majaribio ya wiki mbili katika klabu ya
Sonderjyske inayoshiriki katika ligi kuu ya Dermark, mshambuliaji
Emmanuel Okwi amefaulu majaribio hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Dernmark,
mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea
Yanga amejiunga rasmi na timu hiyo baada ya kufuzu majaribio yake.
Okwi amesaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo na leo
ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari akikibidhiwa jezi
namba 25.

Mpaka
sasa haijawekwa wazi ni kiasi gani klabu ya Simba imelipwa kuumuza Okwi
ambaye miaka kadhaa nyuma walimuuza kwa $300,000 kwenda klabu ya Etoile
Du Sahel ya Tunisia kabla hajarejea Tanzani kuitumikia Yanga.
No comments:
Post a Comment