NaPaul Chengula
MSHAMBULIAJI Mliberia wa Yanga SC, Kpah Sean Sherman (pichani)
anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatatu kwenda Johannesburg, Afrika
Kusini kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu ya
Mpumalanga Black Aces ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Sherman
aliyejiunga na Yanga SC Desemba mwaka jana, amepata nafasi ya kujiunga
na timu hiyo na klabu yake imeridhia aende, baada ya kuleta mshambuliaji
mpya, Donald Ngoma kutoka Zimbabwe.
Sherman
aliyetokea klabu ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini, Cetinkaya FC, ambayo
alikuwa anaichezea kwa mkopo kutoka Aries FC ya kwao Liberia hadi sasa
ameichezea Yanga SC mechi 27 na kuifungia mabao sita tu
No comments:
Post a Comment