Tuesday 28 July 2015

YANGA VS AZAMA WATOLEANA KAULI KUELEKEA ROBO FAINALI,SOMA HAPA



WANAOONGOZA KWA MABAO KOMBE LA KAGAME 2015 

Michael Olunga Gor Mahia 4
Malimi Busungu Yanga SC 3
Salah Bilal  Khartoum    3
Kipre Tchetche Azam FC   3
John Bocco Azam FC 2
Mateo Simon KMKM 2
Mohamed Awad  Shandy 2
Nahimana A.Aziz LLB  2
MAHASIMU wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC na Yanga SC watakutana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Hiyo itakuwa mara ya pili, Yanga SC na Azam FC kukutana katika Kombe la Kagame, baada ya mwaka 2012 kukutana katika fainali pale pale Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Ilikuwa Julai 28, mwaka 2012 katika mchezo uliochezeshwa na refa Thierry Nkurunziza wa Burundi, Yanga SC ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 wafungaji Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 44 na Said Bahanunzi ‘Spider Man’ dakika ya 90 na ushei.
Moja kati ya chachandu za kuelekea mchezo huo ni vita ya ufungaji bora wa mashindano- wachezaji wawili wa kila timu wakiwa kwenye chati ya wafungaji wa mabao mengi hadi sasa kwenye mashindano hayo. 
Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Michael Olunga anaongoza kwa mabao yake manne, lakini 
Malimi Busungu wa Yanga SC na Kipre Herman Tchetche wa Azam FC wanafuatia kila mmoja akiwa na mabao matatu, sawa na Salah Eldin Osman Bilal wa Khartoum N ya Sudan.
Aidha, John Raphael Bocco wa Azam FC ana mabao mawili sawa na Amisi Joselyn Tambwe wa Yanga SC- na wachezaji wote hao wanatarajiwa kuanza keshokutwa timu hizo zikikutana Uwanja wa Taifa.
Busungu, Tambwe, Kipre na Bocco- je nani kati yao atatunisha akaunti yake ya mabao Kombe la Kagame 2015 Jumatano? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

No comments:

Post a Comment