Monday, 31 August 2015

DK SLAA ATEMA CHECHE LEO HII DAR ES SALAAM

KATIBU mkuu wa chama cha CHADEMA,Wilbroad slaa, ameibuka na kutangaza kuwa hii leo atazungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa serena uliopo jijini dar es salaam

 Hatahivyo pamekuwa na maswali mengi juu ya kuwa kimya ambapo wengine wamekuwa wakifikiri amejitoa katika chama hicho kutokana na ujio wa waziri wa zamani wa tanzania  Mh Edward Lowasa,kuingizwa katika chama chao na kuwania uraisi kwa tiketi ya ukawa

  Mapema mwezi ulio pita ilishuhudiwa mwenyekiti wa umoja wa ukawa  Prof Imbahim Haruna Lipumba,kujitoa au kuachia ngazi ya uwenyekiti wa ukawa pamoja na uongozi kwenye chama chake cha CUF na kuwa mwanachama wa kawaida katika chama cha wananchi kafu jambo ambalo lilizua maswali mengi kwa wapenzi na wanachama wa CUF lakini yeye alisema ameona akae pembeni kutokana na kuona mambo waliyo kubaliana yamekuwa yakienda tofauti.

Hii leo watu wanasubiri kwa shauku kubwa kujuwa nini ambacho  Dk slaa anataka kuzungu mza na waandishi wa habari huku kukiwa na taarifa kuwa anataka kurejea kwenye chama chake na kuhakikisha wanalimaliza jambo lililo kuwa wameanza nalo la kuhakikisha kuwa ukawa una chuku wa nchi kama walivyo kuibaliana hapo  awali.

No comments:

Post a Comment