Mchezo wa mpira wa miguu ni miongoni mwa
kazi zenye mishahara mikubwa sana, kama ambavyo mtu kipato chake
kinavyoongezeka ndivyo anavyotamani kumiliki kitu kizuri zaidi… Mastaa
wa soka ni watu ambao wamekuwa na utamaduni wa kumiliki magari mengi na
ya gharama ila kila mtu anapenda gari kulingana na hitaji lake au
mapenzi yake
August 3 nakusogezea gari ambalo linamilikiwa na mastaa wengi zaidi wa soka.
Mastaa wenye urefu kama Peter Crouch hupenda kutembelea Range Rover kwani magari ya chini huwa sio rafiki na maumbo yao. Range Rover ni gari ambalo lina thamani ya zaidi ya dola 60,000/= ambazo ni zaidi ya Tsh 120,000,000/=.
1. Peter Crouch ni staa ambae amewahi kuichezea timu ya Liverpool na sasa yupo katika klabu ya Stoke City.
2. Robin van Persie wengi tulianza kumjua kupitia vilabu vya Arsenal, Manchester United ila kwa sasa yupo katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.. Jamaa nae ana huu mchuma pia aisee !!
- Dareen Bent huyu ni mkali mwingine ambae amewahi kutamba katika vilabu vya Aston Villa, Tottenham Hotspur sasa yupo katika klabu ya Derby County.
5. John Terry ni nahodha wa klabu ya Chelsea lakini pia anaichezea timu ya taifa ya Uingereza.
- Wayne Rooney nahodha wa Manchester United nae yumo katika orodha ya mastaa wanaomiliki Range Rover
- Michael Essien mkali wa soka kutokea Ghana ameingia pia katika hii orodha
- David Beckham hadi anastaafu soka alikuwa anatajwa kuwa mwanasoka tajiri Duniani, akaona sio mbaya na yeye kumiliki Range Rover yake kali kabisa!!
- Mbwana Ally Samatta huyu ni mchezaji pekee wa Kitanzania ambae ameingia katika hii orodha, amewahi kutamba na klabu ya Simba kabla ya kutimkia TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment