Kumekuwa
na taarifa nyingi mfululizo kuhusu kinachoendelea CHADEMA baada ya
kupokelewa kwa Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa… swali ambalo ripota wa CHENGULA NEWS alimuuliza Mbunge Tundu Lissu kuhusu ishu ya mpasuko ambayo iliandikwa sana Magazetini, jibu lake lilikuwa hili >>>> “Haya
maneno ni ya siku nyingi sana na tumetabiriwa maafa tangu siku ya
kwanza… Lowassa hakukaribishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA pekeyake,
Wenyeviti wa UKAWA wote walikuwepo kwenye stage. Anaesema UKAWA
imeteteleka hayo maneno hayataisha” — Tundu Lissu.
Magazeti yameendelea kuandika kuhusu
stori ya kinachoendelea CHADEMA, gazeti la Raia Tanzania August 01 2015
limebeba headline hii >>> “Dk. Slaa ajivua uanachama, ni siku chache baada ya kujiuzulu Ukatibu Mkuu, arejesha nyaraka, gari” >>>
Zitto Kabwe amepost picha ya gazeti hilo @Instagram na kuyaandika haya >>> “Siasa
zinabadilika sana. Siamini kama hili laweza kutokea, lakini wiki kwenye
siasa ni kubwa mno. Sisi wengine tunatazama tu maana tulipita kwenye
changamoto hizi“– @zittokabwe
No comments:
Post a Comment