Saturday, 12 September 2015

CCM WATOBOA MBINU YA UKAWA,KWENYE KAMPENI

Image result for kampeni za ccmMGOMBEA uraisi kwa tiketi ya chama cha cha mapinduzi ccm,John pombe Magufuli,amewataka wa tanzania kuwa makini na kampeni za mwaka huu kutokana na mambo yanayo endelea kujitokeza katika kampeni za sasa hususani kupitia upinzani jambo ambalo limekuwa likitengeneza sura ya chuki miongoni mwa wananchi na viongozi wa vyama vingine

  Hatahivyo magufuli aliifananisha tanzania na libya kutokana na kile kilicho kuwa kikitengeneza siasa za chuki miongoni mwa wanasiasa,pia ameshangazwa na mfumo wa wapinzani kumfuata katika mikoa ambayo wao kama ccm wamekwisha kuipita jambo ambalo limekuwa likichukua tafsiri mpya miongoni mwa wanasiasa na wananchi.

MIONGONI mwa wanasiasa  Tanzania wamekuwa wakichambua siasa ya tanzania na kusema kuwa kwa sasa siasa Tanzania imekuwa na sura tofauti kwakuwa kila kijana anaijuwa siasa kuliko au tofauti na  miaka mingine ambapo vijana wengi wamekuwa hawataki kujihusisha na mambo ya siasa

MAGUFULI amewataka watanzania kuchukuwa uwamuzi wa kumpa nafasi ya kushika dola kwani yeye ndo mkombozi wa nchi na kuwaahidi walimu kupata vitendea kazi ikiwemo kila mwalimu kuwa na laptop ya kufanyia kazi mashuleni

No comments:

Post a Comment