
Berto alikuwa moto lakini Mayweather, aliyekuwa akitetea mataji

Mayweather, 38, alizawadiwa alama 120-108, 118-110 na 117-111 kwenye pigano hilo lililoandaliwa ukumbi wa MGM Grand usiku wa kuamkia Jumapili.
Mayweather amesisitiza kuwa hilo litakuwa pigano lake la mwisho, lakini ikizingatiwa kwamba amefikia rekodi ya Rocky Marciano ya kupambana na kushinda mapigano 49-0, huenda akaamua kuongeza.
"Maisha yangu ya uchezaji yamefikia kikomo, hilo ni rasmi,” alisema Mayweather ambaye sasa ni bingwa wa ndondi katika vitengo vitatu tofauti vya uzani.
Bondia huyo anachukuliwa sana na wengi kuwa stadi zaidi katika kizazi chake.
"Lazima ujue wakati wa kuacha. Sasa nakaribia umri wa miaka 40. Sijabaki na chochote cha kuthibitisha kwa ulimwengu wa

Berto, 32, ni bingwa mara mbili wa dunia uzani wa welter na aliingia kwenye pambano hilo akiwa amewahi kupoteza mara tatu pekee katika mapigano 33 ya kulipwa aliyoshiriki.
Mayweather aliyekuwa akipigania ubingwa wa dunia mara ya 26 hajawahi kushindwa tangu 1996.
Iwapo ataamua kutostaafu, wengi wanatarajia huenda akaamua kukabiliana tena na Manny Pacquiao mwaka ujao.

Aidha, anaweza pia akashawishika kukutana na mshindi wa pigano la Novemba 21 kati ya Miguel Cotto na Saul Alvarez
No comments:
Post a Comment