Saturday 10 October 2015

JINA LA GNAKO LATUMIKA NA WIZI

Leo CHENGULA NEWS kapiga stori na mmoja wa mashabiki wa kundi la Weusi Deo ambaye amedai kutapeliwa na mmoja wa wasanii wa kundi hilo Gnako.

Amesema anafahamu Weusi wanafanya biashara ya kuuza bidhaa zenye nembo yao..aliona post moja aliyoweka Gnako kwenye mtandao wa Facebook, akaipenda na kutaka ainunue, aliambiwa alipie kwanza pesa nusu na baada ya muda alimtumia 52,000 akitaka kupewa moja ya product zao.
Baadaye akamtumia ujumbe wa kutaka amalizie ili atumie bidhaa yake na alifanya hivyo kwa kuwa alikua akimwamini sana, kilichotokea anasema baada ya muda alishangaa Gnako amemblock kila mahali na akaamini ametapeliwa.

Gnako amezungumza na kusema wao hawafanyi biashara kwenye mitandao ya kijamii na iyo issue iyo si ya kweli na aliyemtapeli si yeye.

No comments:

Post a Comment