Guardiola amezungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mechi na Barcelona kesho
Baada
ya kufungwa mabao 3-0 katika Nusu Fainali ya kwanza Barcelona Mei 6,
kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 anatakiwa kushinda 4-0 nchini
Ujerumani ili kutinga Fainali.
Lakini
alipoulizwa kuhusu ofa ya Manchester City, mchezaji na kocha huyo wa
zamani wa Barca, alisemna; "Vijana, nimesema hii mara 200 kwamba nina
Mkataba wa mwaka mmoja zaidi hapa. Msimu ujao nitakuwa hapa, ni hivyo tu,".
Guardiola
aliiacha timu yake kipenzi Barcelona mwishoni mwa mwaka 2012 baada ya
kushinda nayo mataji 14 yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya
mwaka uliofuata kujiunga na Bayern na tangu hapo ameiwezesha kushinda taji la Bundesliga mfululizo.
No comments:
Post a Comment