Na Paul Chengula
Ni kweli kwamba uko kwenye mapenzi mazito na Mose Iyobo ambaye ni dancer wa Diamond Platnumz? ……………Waandishi wengi walikua wanauliza hili swali kwa Aunty na jibu lake lilikua linaishia kuwa moja tu >>> ‘hata mimi mwenyewe hizo habari nazisikia kama mnavyozisikia nyie, ila baba wa huu ujauzito namjua mwenyewe‘ CHENGULA NEWZ, imepata nafasi ya kukaa kwenye Exclusive interview na Mose Iyobo anaeonekana mwenye furaha mara nyingi, baada ya kuulizwa kama ni kweli yeye ndio baba Kijacho akaanza kwa kusema >>> ‘Ndio iko hivyo, si unajua mahusiano ni sehemu yoyote hata kwenye daladala yanaanza’
Kwenye sentensi ya pili Mose amesema uhusiano wao wa kimapenzi ulianzia wakati wakiwa kwenye tuzo za MTV Durban South Africa June mwaka 2014, walikutana huko na wakajuana huko.
‘Kwa hivyo tulivyofikia tumekubaliana tu mimi nitakua Baba na yeye atakua mama tuendeleze mwendelezo wa huyo anaekuja‘
No comments:
Post a Comment