Sunday, 24 May 2015
RONALDO AIKACHA REAL MADRID
PSG imetajwa kuwa ni club ambayo inalipa mishara mikubwa wachezaji wake lakini bado ina nia ya kuendelea kupelekea majina makubwa kwenye club yao.
Gazeti maarufu la kupata udaku wa Michezo Marca limeripoti kwamba Paris Saint-Germain wamefikisha maombi yao kwa timu ya Real Madrid kwamba wanamtaka mchezaji Cristiano Ronaldo kwa ada ya €125 million. Lakini gazeti hilo limesema kwamba Ronaldo angependa kuona mkataba wake unaisha ambao unafka hado 2017-18.
Pia limeongeza kwamba Ronaldo anataka kuongea na Rais wa Real Madrid Florentino Perez kuhusu future ya club hiyo. Mipango na mambo mengine ili timu iweze kuchukua makombe. Sasa je majibu atakayo toa Perez yatamfurahisha Ronaldo na kumpa matumaini ya kubakia au ataondoka?.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment