Nimezaliwa 28 September, Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa
mwisho, nina dada watatu. Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili
yupo hapa hapa, ameolewa ana familia yake. Wa kwanza yuko kule anafanya
kazi ana mtoto mmoja. Wa tatu yuko kule anasoma na anafanya kazi.
MIAKA MITANO KABLA YA MWAKA 2006, WEMA ALIKUWA NI MSICHANA WA AINA GANI?
Wema alikuwa ni msichana wa kawaida. Wakati ule ulikuwa ukiniuliza unataka kuwa nani ukikua ningekujibu nataka kuwa air hostess sababu dreams zangu zilikuwa ni kuwa air hostess, sijawahi kufikiria kabisa kuingia kwenye fame. Though nilikuwa nawaangalia watu kama Ray C, K-Lynn, Kwasababu mimi nilikuwa nasoma academic na shuleni kwetu nakumbuka tulikuwa tukitoka ile home time kulikuwa na duka fulani hivi la mpemba tunaenda tunakula sambusa nini, so magari yatapita nini and we would see Ray C and everybody will go like ‘you see Ray C’ you know, kwahiyo we go crazy over superstars na watu famous.
Kiukweli I never so myself kuwa katika this position ambayo niko. Kwahiyo nilikuwa tu msichana ambaye sina ndoto za kuwa star lakini nilikuwa tu nawashangaa masupastaa. My dad amekuwa anapenda sana mashindano ya Miss Tanzania and kila mwaka alikuwa anamake sure kwamba amenunua tiketi ya kwenda kuangalia Miss Tanzania.
So nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa akina Sylvia Bahame tumekaa nyumbani amekosa tiketi. Akakaa akasema ‘kumbe ukiwa umekaa nyumbani ndio unaenjoy vizuri kuliko hata kwenda pale’ akasema ‘one day nawish one of my beauties hata kama hatoshinda, nikilipia tiketi naenda nikijua kabisa nimeenda kumlipia binti yangu.
So sikukiweka kichwani hicho kitu lakini after kuingia katika whatever na nini, so siku nimekaa na dad nikamwambia ‘dad unakumbuka kuna siku ulisema hivi’ akasema ‘yes I remember’ . Hata Mange Kimambi alivyokuja kuniapproach, alivyoniona Sleep Way akaniambia kwamba anataka niingie katika mashindano, nikamwambia kwamba mimi nina wazazi wangu, siwezi nikaamua tu mimi mwenyewe na mimi nakaa na wazazi, so nilivyoongea na mama akasema ‘ongea na baba yako’ nikampigia simu baba alikuwa kipindi hicho Dodoma, akaniambia ‘fanya my beauty nitakusupport’, hakuthink twice alinipa go ahead kabisa.
No comments:
Post a Comment