Na Paul Chengula.
YANGA imetenga dau la Sh797 milioni ili kusuka
kikosi kipya ambacho kitadumu kwa misimu miwili ijayo na kufanya vizuri
zaidi kwenye michuano ya kimataifa kuanzia na Ligi ya Mabingwa Afrika
mwakani.
Katika msimu uliomalizika ilitumia karibu Sh500 milioni tu.
Tayari katika kiasi hicho, zimeshapungua fedha
zilizotumika kwenye usajili wa nyota wawili wa kigeni Mbuyu Twite na
Haruna Niyonzima.
Jopo la usajili wa Yanga limepania kusuka kikosi
ambacho kitakuwa imara zaidi na ambacho kitakuwa na mtazamo mpya na
tayari Mwenyekiti wa klabu ambaye ni Bilionea Yusuf Manji ameunga mkono.
Habari za ndani ambazo Mwanaspoti imejiridhishwa
nazo, zinasema kwamba usajili wa Yanga umepanga kunasa wachezaji wote wa
maana wa ndani yakiwemo majina yaliyopendekezwa kama viungo Haruna
Chanongo ambaye ni huru na Deus Kaseke wa Mbeya City.
Fungu hilo la Yanga litatumika pia kwenye
maandalizi ya kambi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa,
tayari imefahamika kwamba Niyonzima amechukua dola 60,000 (Sh120
milioni) katika mkataba wake wa miaka miwili huku pia Twite akichukua
dola 30,000 (Sh60 milioni) akisaini mkataba wa mwaka mmoja.
“Ukiangalia kiasi hicho utaona ni kikubwa sana kwa
usajili, lakini pia tunataka kitumike katika kulipia gharama ya kambi
yetu ambayo tumepanga itaanza Juni 9 baada ya kocha wetu kurudi Juni 7
mwaka huu,” kilisema chanzo chetu.
Katika harakati hizo za usajili, Yanga imetamka
kwamba kwa sasa usajili wa wachezaji wao wa kigeni utalazimika kusubiri
mpaka keshokutwa Jumamosi ili kupata majibu ya maombi yao ya ongezeko la
idadi kutoka watano wa sasa hadi kumi lililowasilishwa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
“Hatutaanza kufanya lolote katika usajili wa
wachezaji wa kigeni tunasubiri kwanza kusikia nini maamuzi ya TFF katika
maombi yetu ya kuwaongeza wachezaji wa kigeni,” aliongeza kiongozi
huyo.
Azam yasubiri kocha
Azam imetangaza kusimamisha zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao.
Uongozi wa timu hiyo umetangaza maamuzi hayo kwa
kutaka kusubiri uteuzi wa kocha mpya wa kuinoa timu hiyo, huku majina
matatu yakiwa mezani yakijadiliwa
No comments:
Post a Comment