MIMI Siyo mfuatiliaji sana wa Muziki wa Kizazi kipya,huwa nakereka Pindi ninaposkiza. Nikiri tu kuwa Mimi Ni Mpenzi Mkubwa wa Muziki lakini siyo Muziki wa kizazi hiki Kipya.
Napenda Sana Kusikiliza Miziki iliyonizidi Umri kama wa akina Marijani Rajabu,Hemed Maneti,Mmbaraka Mwinshehe na wengeni wenye akili Timamu wa miaka hiyo kama hao.
Kadhilika Mimi Siyo Mpenzi wa `magazeti ya Udaku` huwa nayaona Mezani huko Majiani lakini sinunui na Ninazidi kumuomba Mungu asinipe ujasiri wa kuyanunua.
Mimi Siyo Mfuatiliaji wa sanaa za wasanii wa kizazi hiki Kipya. Hivi Karibuni niliona Picha ya Msanii anayeitwa `Shilole` samahani kama ntakuwa nimekosea jina hilo. Niliona Picha za Dada huyo anayejitaa `msanii` wa Tanzania akiwa nusu Mtupu huko Nje ya Nchi nadhani ni Ubelgiji. Kuanzia kiunoni kwenda Juu alikuwa wazi kwa maana hakuwa na Nguo ( Asstaghaffirulahy)
Huku Chini alikuwa na Nguo Nyepesi iliyoonyesha mauongo yake ya Ndani ambayo huenda pia hakuvaa Nguo ya Ndani. ( MUNGU TUNUSURU WAJA WAKO)
Alikuwa Jukwaani akinengua na alikuwa akinengua Mithili ya mja aliyezidiwa na `mahaba` akiwa faraghani.
Alichokifanya Msanii huyo naambiwa siyo mara ya kwanza anafanya hivyo ( ni mzowefu wa kukaa uchi) Kama Ndivyo yawezekana kabisa huyu Mwanadada anafanyabiashara ya `kuuza mwili wake` Lakini anatumia `kimvuli` cha usanii kujitangaza ili azidi kupanua Soko la Biashara yake haramu. ( HANA DINI HUYU? HANA WAZAZI AU WALEZI HUYU? )
Wanaofuatili Nyimbo zake wanasema katika moja ya Tungo zake aliwahi kusema hawezi kuhama Dar es salaam na anafanya chochote ilimradi apate tu Fedha`( hao Ndiyo wasanii wa Tanzania) Wimbo huo unamfundisha Nini Kijana?? Upuuzi uliyopevuka.
Naambiwa kuwa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kabla ya tukio hilo huko Nyuma liliwahi kumwita msanii huyo na kumuonya juu ya Tabia yake ya kukaa `uchi` majukwaani na aliomba Radhi,karudia tena na tena na tena ( HUYU SIYO MUHUNI ANAYEJIUZA HUYU!!!)
BARAZA LA SANAA LA TAIFA ( BASATA) ambalo Ndilo lenye dhamana ya kusimamia sanaa na Burudani Nchini limeendelea kumuangalia Msanii bila kumchukulia hatua yeyote zaidi ya Kumuonya tu.
Ninamshukuru Mungu sana kwakuniepusha na hiki kinachoitwa sanaa ya kizazi kipya,Ningekutana na watu kama hawa akina `shiloli` wanaofanya jitihada za kuichafua Tanzania yetu katika Sura ya Dunia.
Nilimsikia Huyu msanii `mkaa uchi` akisema anasikitishwa na kilichotokea na anamlaumu aliyempiga hizo picha na kuzisambaza. ( NDUGU ZANGU HUKU DUNIANI KUNA VICHAA WANAOTEMBEA WATUPU MAJIANI,HUYU MSANII NINI KITAMTOFAUTISHA NA MWENDAWAZIMU??) ANAVUTA BANGE? ANAJIUZA? ANAUZA MADAWA YA KULEVYA AU KATUMWA KUTUHARIBIA NCHI YETU??)
Kama `Shiloli` anajiuza basi aendelee kujiuza kimya kimya na ajitangaze kwa njia Nyingine lakini syo kwa watanzania wote. Watoto wetu tutawaficha wapi wasiambukizwe tabia hizo na huyo `mwendawazimu?
Katika kudhihirisha `uwendawazimu wake`` msanii huyo alikuwa anahoji ni kwanini amedhalilishwa kwakupigwa picha? Hivi Nduhu unayesoma hapa huyu Dada atakuwa Mzima kweli? Kadhalilishwa au kajidhalilisha? Kaambiwa anajiuza au kajitangaza anajiuza ?
Hivi unaweza kutembea Mtupu majiani mbele ya hadhara alafu ukauwauliza waliyokutazama ni kwanini wanakudhalilisha? Kwa wanaomfahamu toka akiwa mDogo naomba mtuelezea kama msanii huyo alishawahi kuugua `uchizi. Au alishawahi kuadhirika na madawa ya kulevya! Tukipata jibu kuwa Ni kweli basi apatiwe matibabu ili arejee ubinadamu kwakuwa tabia anazofanya zinapaswa kufanywa na `wanyama`.
Ni lazima Vyombo vinavyihusika vimchukulie hatua kali sana ikiwa ni pamoja na kumfutia leseni na kutokumpa kibali cha kujiita msanii kutoka Tanzania pindi anapofika Nje ya Nchi.
Asituletee tabia zake zilizoshindikana hapa kwetu kwakuwa wapo watoto wanaolelewa kama maadili mema asije kuwachafua kama alivyojichafua yeye na akifanya jitihada za kuichafua Tanzania yetu.
Mungu azidi kunipa Nguvu kupambana na uovu kama huu wakipuuzi.
Duu ila itakuwa fundisho kwa wasanii wote
ReplyDelete