Friday, 15 May 2015

SIMBA SC YAPATA PIGO LINGINE


Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Stephene aliingia madarakani mwaka jana mara baada ya uongozi kuingia madarakani kuiongoza timu hiyo chini ya Rais Evans Aveva.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Stephene amesema kikubwa kilichomfanya ajiuzulu ni kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo.
Katibu huyo alisema madaktari wa Hospitali ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ndiyo waliomshauri apumzike kwa muda usiojulikana kutokana na ugonjwa unaomsumbua baada ya kufanyiwa vipimo.
“Cha kwanza kabisa katika mwili wa binadamu ni afya na hayo mengine yanakuja baadaye, madaktari wamenishauri nipumzike kufanya kazi kwa muda usiojulikana kwa ajili ya kujiuguza kwanza. Ugonjwa sitaweza kuutaja kwa sasa, tayari nimekabidhi barua kwa uongozi.

“Ninaomba nichukue muda huu kuwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki kwa jumla kwa kipindi chote nilichokuwa ninaiongoza Simba,” alisema Stephen

No comments:

Post a Comment