Na
Paul Chengula
KAMATI
ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoketi Jumanne
tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Jerry Muro (pichani juu) kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.
Akitoa
utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia
kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa
michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa
kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza
faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi
wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya
matamshi ya aina hiyo.
Shitaka
linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa
kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC, Juuko Mursheed, na kiongozi wa
Friend Rangers, Hery Chibakasa wa Friends Rangers kuhamasisha vurugu
katika mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea Januari 29,
2015, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine
itakapopangwa.
Kamati
iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred
Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na
Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosbabishwa na mgomo
wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.
No comments:
Post a Comment