Tuesday, 5 May 2015

YANGA KUKABIDHIWA KOMBE

Kocha (1)Na. Paul Chengula, Dar es salaam
Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara, Klabu ya Dar es salaam  Young Africans inatarajia kukabidhiwa kikombe chake cha ubingwa siku ya jumatano baada ya mchezo dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kaimu Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Fatma Abdullah amesema kuwa wameamua kuipatia Yanga kikombe cha Ubingwa siku hiyo ikiwa ni kabla ya mchezo mmoja ili kumalizika kwa ligi hiyo kufatia kuwa mchezo wa mwisho watakuwa ugenini Mtwara huku Jumatano watakuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani.
“Tumewasiliana na Wadhamini Vodacom hivyo Siku hiyo Yanga tutawakabidhi kombe lao, Tumefanya hivyo kwasababu watakuwa katika Uwanja wao wa Nyumbani kama unavyojua mchezo wa mwisho watakuwa Mtwara” Amesema Fatma Abdullah.yanga muro
 Yanga wamefanikiwa kuibuka Bingwa wa VPL kwa msimu wa 2014/2015 baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika ligi huku wakiwa na michezo miwili mkonono ukiwemo huo wa jumatano dhidi ya Azam FC ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi huku hadi sasa wakiwa hawana uhakika wa kupata hata nafasi ya pili ambayo inawaniwa pia na Simba SC.

No comments:

Post a Comment