Monday 1 June 2015

Breaking newz: AZAM YAZIPIKU SIMBA NA YANGA KWEYE USAJILI

AZAM FC imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mkali wa mabao wa Mtibwa Sugar, Ame Ally (pichani kushoto).mkali huyo alikuwa akiwaniwa na vigogo wa timu za simba na yanga ambao walitaka kuipata sain ya mchezaji huo ambae amefanikiwa kuzifunga zote katika vipindi tofauti
 
Ame amesaini Mkataba wa miaka miwili na Azam FC baada ya msimu mzuri akiwa na timu ya Manungu, Turiani, mkoani Morogoro.

Pia  alikiri kufwatwa na   simba pamoja na yanga kwa wakati tofauti lakini walishidwa kuununua mkataba ambao bado ulikuwa mbichi kwenye timu ya mtibwa ,pia ametoa pongezi kwa timu ya azam kwa kitendo walicho fikia cha kuununua mkataba wake na kusema kuwa simba na yanga wanataka wachezaji walio huru jambo ambalo sisawa katika mpira ukimtaka mchezaji lazima utumie garama kumpata'

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema; "Tupo kwenye mazungumzo na klabu yake, yule mchezaji bado ana Mkataba na Mtibwa, hatujamalizana,"amesema.
. 
Ame ambaye msimu huu ametikisa nyavu za vigogo wote, Yanga, Simba na Azam ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na Mtibwa Sugar kiasi cha kuzivutia timu nyingi nchini

Imekuwa bahati yao Azam FC wameinasa saini ya mshambuliaji huyo mrefu mkali wa vichwa na mwenye mashuti makali.

Kusajiliwa kwa Ame, kunaifanya safu ya ushambuliaji ya Azam FC isheheni kisawasawa, kwani tayari inao wakali kama Kipre Tchetche, John Bocco, Didier Kavumbangu na Gaudence Mwaikimba.

Azam FC ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu nyuma ya Yanga SC waliobuka mabingwa.
Mwakani, mabingwa hao wa zamani watacheza Kombe la Shirikisho la Afrika.

No comments:

Post a Comment