Monday, 1 June 2015

TOMAS ULIMWENGU AWADUWAZA WA MISIRI

Thomas Ulimwengu kushoto akitafuta maarifa ya kumtoka mchezaji wa Lupopo jana
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya FC Lupopo katika michuano maalum ya kirafiki, iliyoandaliwa na mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi.
 
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa TPM, Ulimwengu aling’ara mno na kufunga mabao mawili mazuri, huku mengine yakifungwa na Cheibane Traore na Adama Traore.
 
Mabao hayo ya Ulimwengu ambaye Lubumbashi anaitwa Rambo, ni salamu kwa Misri ambayo itacheza na Tanzania katikati ya mwezi huu katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.

Akizungumza na CHENGULA NEWZ, kwa simu kutoka Lubumbashi leo, Uli ‘Rambo’ alisema; “Nimefurahi sana nimefunga mabao na kuisaidia timu yangu, lakini kikubwa nafurahi nipo katika kiwango kizuri kuelekea mechi yetu na Misri,”amesema.

No comments:

Post a Comment