Chris Brown anaziandika headlines kwa mara nyingine tena, siku chache zilizopita staa huyu alikuwa Ufilipino kwa ajili ya kufanya show, lakini akazuiliwa kuondoka nchini humo jana kutokana na mzozo wa mkataba wake wa nyuma.
Chris Brown alizuiliwa Airport siku ya Jumatano asubuhi akiwa anajiandaa kuondoka na ndege yake binafsi kutoka Manila International Airport kwenda Hong Kong kwa ajili ya concert nyingine.
Chombo cha Sheria na Haki Ufilipino ilitoa amri siku ya Jumanne usiku kumzuia Chris Brown kuondoka nchini humo mpaka atakapolipa hela za Promoters walioandaa show kipindi cha mwaka mpya, show ambayo Chris hakutokea.
Kwa sasa Chris Brown ameambiwa
kama atahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu za msingi basi itambidi
aombe ruhusa kwa Ofisi ya Uhamiaji ambao kama wakikubali basi watampatia
cheti kinachoonyesha sababu hizo ni za mzingi na kuwa atarudi.
No comments:
Post a Comment