Wednesday 26 August 2015

LOWASA MIKONONI MWA POLISI DAR

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku wagombea wa vyama vya siasa kufanya vitendo vinavyo hatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kufanya mikusanyiko isiyo rasmi kwenye masoko na vituo vya daladala.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.. ‘Sasa kuna jambo limejitokeza ambalo limetulazimisha sisi jeshi la Polisi kupiga marufuku wagombea mbalimbali wa vyama katika uchaguzi huu hususani wale wenye nafasi ya Urais kwa vitendo vyao au kwa mtindo ambao umeibuka sasa hivi wa kwanza kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kama vile vituo vya Daladala, Masoko, ndani ya Daladala au Mabasi yoyote yale – Kova
.
‘Na hii inasemakana kwasababu ya kujua matatizo ya watu ambao wenye kipato cha chini inawezekana nia ni nzuri sana lakini sisi hapa atuzungumzia siasa au Uchumi  hapa tunazungumzia suala la Usalama kutokana na uzoefu uliojitokeza kwa zoezi hilo ni kwamba hilo zoezi sio la rasmi pia ziara hizo zinasababisha mikusanyiko mikubwa  isiyo ya lazima katika hali ambayo inaashiria kutokuwepo kwa Amani – Kova
.
‘Wakati wa ziara wa aina hizo wamejitokeza makundi tofauti ya watu wakiwemo, waendesha Bodaboda wengi,  watu wa Daladala wengi wanajitokeza sawa wanashangilia  lakini kwa watu wengine ambao wasio wa makundi hayo ni kwamba inakuwa inaleta taharuki, hofu,  usumbufu, kuna kuwa na makelele mengi,  msongamano wa magari,  au hata kusimamisha usafiri katika  eneo hilo ambalo mgombea anakuwepo nasema kwamba inawezekana huyo mgombea kuna faida anayoipata lakini yeye kupata faida peke yake haitoshi kama suala la usalama alizingatiwa’ – Kova
.
‘Kwa mfano leo tarehe 25 mwezi wa nane ilibidi RPC wa kamanda Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya alilazimika kukutana ana kwa ana na Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa saa sita mchana watu walikuwa wamejaa pale katika mtaa wa Congo nadhani na Uhuru misongamano ya Magari mengi, Pikipiki wananchi wakalalamika kwamba ni nini sasa kinatokea na unajua Dar es Salaam ukisimamisha magari  kutokana na kundi lako kubwa basi litawaathiri Wananchi’ – Kova

No comments:

Post a Comment