Tuesday, 1 September 2015

UKAWA WAMJIBU SLAA HII LEO DAR ES SALAAM,MENGINE YAIBUKA

UMOJA wa ukawa umeibuka na kukanusha vikali maneno ya alie kuwa mwanachama na katibu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA,  Dr Wilbroad Slaa,kwamadai ya kuwa kwasasa hawawezi kujibu chochote kutokana na anae watuhumu sio mwanachama wala sio mpenzi wa siasa kwa sasa.

Hatahivyo wapenzi na wanachama wa umoja huo wamekuwa wakilizungumzia swala hili  la aliekuwa katibu mkuu wa  chama hicho slaa kuwaita wenzie makapi wakati hata yeye alikuwa ni kapi baada ya kuachana na chama zake cha zamani ambacho ni ccm na kujiunga na chadema .

Mmoja wa wanachama hao ajulikanae kwa jina la, Joshua bryson,alikuwa na haya yakusema alipo kutana na CHENGULA NEWS mapema hii leo jijini dar es salaam,

"kiukweli  sisi kama wanaukawa hatuogopi kauli zake za vitisho kwani tunaelewa lengo lake nikuja kwenye kipindi hiki cha kampeni na kutaka kuwavuruga wanachama ili kuto kufikia lengo la umoja wa ukawa,kila mtu anajuwa yakuwa hakuna mtu aliekuwa na ushawishi mkubwaa kama Prf Imbahim Lipumba,lakini leo kaondoka na bado chama cha CUF kipo imara hivo kuondoka kwake yeye kwetu haimaanishi chama kitakufa  kwakuwa chama sio cha mtu mmoja.

Hatahivyo viongozi wa umoja huo wameibuka na kusema kuwa kama slaa angekuwa mzalendo angekuja na orodha ya mafisadi wote tanzania na kuwa taka watanzania kuchukua uamuzi wenyewe na si kuibuka na kuanza kumshambulia mgombea mmoja jambo ambalo watu wamekuwa  wakilichukulia kama nimiongoni mwa watu walio tumwa.

No comments:

Post a Comment