Wednesday 30 March 2016

MWINYI KAZIMOTO AFUNGUKA HII LEO

Na Paul Chengula, DAR ES SALAAM
KIUNGO mkongwe wa wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto Mwitula, anayechezea Simba SC ya Dar es Salaam amesema kwamba wachezaji chipukizi wa sasa sasa wengi hawashauriki.
Akizungumza na CHENGULA NEWS – ONLINE Jijini Dar es Salaam jana, Kazimoto amesema kwamba wachezaji vijana wadogo wa siku hizi ni wajuaji na mambo ya mitandao ndiyo yanawaharibu .
“Huwezi kumshauri kijana wa siku hizi akakuelekwa, kwanza ataona unamuonea wivu, na haya mambo ya mitandao tena, wakisifiwa kidogo wanajua, basi inakuwa tabu,”amesema.
Kazimoto amesema kwamba inakuwa vigumu kwao wachezaji wakongwe kuwashauri vijana hata wanapoona wanakwenda ovyo na wanaweza kujiharibia maisha yao ya soka, kwa sababu ni viburi.

“Tumebaki kuwaangalia tu, atakayeweza kujitambua mwenyewe na kujua anakosea, atakuja kwetu wakubwa tumpe ushauri,”amesema Kazimoto. 
Kazimoto alikuwa anazungumzia nidhamu na maadili ya wachezaji nyota chipukizi kuanzia ndani na nje ya Uwanja, ambavyo kwa kiasi kikubwa haviridhishi.

No comments:

Post a Comment