Genk imecheza mchezo wake wa pili na kulazimishwa kucheza kwa dakika 120 na baadae mikwaju ya penati, dakika 120 zilimalizika kwa Buducnost kuongoza kwa goli 2-0, goli ambazo zilifungwa na Djalovic dakika ya 2 na Raickovic dakika ya 40 lakini mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati kutokana na KRC Genk kuibuka na ushindi kama huo katika mchezo wao wa kwanza
.
Katika mikwaju ya penati Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa penati 4-2, penati za ushindi wa Genk
zilipigwa na nahodha wao Thomas Buffel, Heynen, Mbwana Samatta na Walsh, hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk itacheza round ya pili ya Europa League dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland.
No comments:
Post a Comment