Friday 15 July 2016

SHAA AFUNGUKA KUJITOA MJ RECORDS

Ni July 15, 2016 ambapo Malkia wa uswazi, Sara Kaisi aka Shaa amefunguka kupitia  chengula news na kuelezea sababu za kuondoka kwenye uongozi wake wa zamani.
Akizungumza na chengula news staa huyo alisema…’Nimekuwa na ndoto ya muda mrefu kama ya miaka mitano iliyopita tumeona wasanii ambao niliokuwa nao MJ Records wakina Izzo Bizness amesimama mwenyewe ukija kwa Quick Rocka nae kafungua studio kwahiyo huu ni muda wangu’Shaa
‘Maamuzi ya mimi kwenda kwenye uongozi wakina Tale ilikuwa baada ya mimi mkataba wangu kumalizika kwenye lebo ya Unity Entertainment ya AY nilifanya nao kazi nzuri mpaka zingine zikakubalika ila maamuzi yangu kwa 2016 kazi zangu zitasimamiwa chini ya record label yangu’- Shaa

No comments:

Post a Comment