Monday 28 September 2015

LOWASA LAIVUU

MGOMBEA wa uraisi kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowasa, amesema kuwa yeye anamwamini mungu kwa kila jambo na ndio maana alienda kwa mchungaji tb joshua kuombewa ili ashinde kwenye uchaguzi mkuuu.

TB joshuwa,alisema kuwa lowasa alikuja kwenye kanisa lake kwa malengo ya kutaka maombi ili afanikiwe kwenye mambo yake hususani katika swala la kugombea urais wa jamuhuri ya muungano ya tanzania mapema mwaka huu

Miongoni mwa wananchi ambao wamekuwa na imani tofauti juu ya kiongozi huyo kuelekea Nigeri na kuombewa na mchungaji huyo mwenye umaarufu wa pekee barani Africa ,wamesema kuwa ni sawa na kutaka kuingia ikulu kwa kila njia jambo ambalo limezua mawazo na mitazamo mingi kwa wananchi

 
TB Joshua,alimtabiria kiongozi huyo wa ukawa kuwa atafanikiwa kuwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania jambo ambalo limekuwa gumzo kwa hivisasa juu ya nani atakuwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania


Serikali imewataka watanzania kujitokeza kwa wingi isiku ya kupigakura ili kufanikiwa kumchagua mtu sahihi wa kuiongoza Tanzani

No comments:

Post a Comment